Akizungumza huko Bandar Abbas jana Alhamisi na wanajeshi wa majini na familia zao, Admeli Irani amesema nguvu za kijeshi za Iran zipo katika ubora wake, na operesheni zake za hivi majuzi zinaashiria hadhi na nafasi yake katika uga wa kimataifa.
Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Iran amesisitiza juu ya kutambuliwa duniani kote uwezo wa Jeshi la Majini la Iran, na kuongeza kuwa ushawishi wao unavuka mipaka ya nchi hii na unatambulika duniani kote.
Kadhali amesema Jeshi la Wanamaji la Iran hivi sasa linatambuliwa kuwa lenye nguvu kubwa na hata maadui zake, akisisitiza juu ya utayarifu wa kikosi hicho iwapo kutatokea mizozo ya moja kwa moja ya baharini.
Amesema kuwa baada ya Mapinduzi ya Kiislamu, Jeshi la Iran limepata kutambulika duniani kote kwa uwezo wake, na uwezo huo umeyapa changamoto mataifa makubwa duniani ikiwemo Marekani.
Hali kadhalika kamanda huyo mwandamizi wa Jeshi la Iran amesema uwezo huo umetokana na msingi wa kiitikadi na doktrini ya kijeshi ya Iran, akisisitiza kuwa Vikosi vya Ulinzi vimejitolea kuwahudumia wananchi wa Iran.
Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Iran amesisitiza sifa ya kimataifa ya vikosi vya wanamaji vya Iran, akibainisha kuwa athari zao zinafika nje ya mipaka ya nchi na zina umuhimu mkubwa duniani kote.
342/
Your Comment